;

Ndindi Nyoro akosoa mpango wa uuzaji wa hiza kwa umma wa KPC

Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro. [Wilbrforce Okwiri, Standard]

Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro amekosoa mpango wa uuzaji wa hisa kwa umma (IPO) wa Kampuni ya Kenya Pipeline (KPC), akidai kuwa haukuendeshwa kwa misingi ya soko na hivyo kuufananisha na kushindwa.

Akizungumza jijini Mombasa wakati wa mkutano wa 11 wa Chama cha Wahasibu Wanawake wa Kenya (AWAK) kuhusu Uongozi na Uwajibikaji wa Wanawake mwaka 2026, Nyoro amesema serikali ililazimika kuwasiliana na Uganda ili inunue sehemu ya hisa za kampuni hiyo.

Kwa mujibu wa Nyoro, hatua hiyo inaonesha kuwa mahitaji ya hisa hizo hayakutokana na soko la kawaida.

Amedai kuwa wakati IPO ilipofungwa, kiwango cha usajili kilikuwa chini ya asilimia tano, huku Uganda ikidaiwa kununua asilimia 21 ya hisa zilizotolewa.

Mbunge huyo pia aikosoa Hazina ya Malipo ya Uzeeni (NSSF) kwa kutumia fedha za wanachama kununua hisa za kampuni hiyo, akisema huo ulikuwa uwekezaji usiofaa.

Ameongeza kuwa wadhamini wa hazina hiyo walipaswa kutumia fedha zao binafsi badala ya fedha za wafanyakazi.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Kampuni ya Kenya Pipeline, mpango huo wa IPO ulifunguliwa Januari 19 na kufungwa Februari 24, 2026, na ulisajiliwa kwa asilimia 105. 7.

Taarifa ya kampuni hiyo inaonyesha kuwa jumla ya hisa shilingi trilioni 11,812,644,350 zilitolewa kwa bei ya shilingi tisa kila moja, huku idadi ya hisa zilizoombwa kufikia shilingi trilioni 12,486,78,724, kiwango kinachoashiria usajili uliopita wa idadi ya hisa zilizotolewa.

.

RELATED NEWS